Monday 10 December 2012

Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe • Biskuti

Vipimo Unga wa ngano 1 Kilo Siagi ¼ kilo Mayai 2 Kastadi (custard) 3 vijiko vya supu Baking powder 1 kijiko cha chai Maziwa 1 ½ gilasi Mafuta Ya kukaangia kiasi katika karai Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 1. Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder. 2. Tia siagi uchanganye vizuri. 3. Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana. 4. Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake. 5- Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana. 6- Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira. Vipimo Vya Shira Sukari ½ kilo Hiliki ilosagwa 1 kijiko cha chai ‘arki (rose flavor) 5 matone Maji 1 gilasi Namna Ya Kutyarisha 1. Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito. 2. Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na ‘arki . 3. Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari

No comments:

Post a Comment